
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 10, 2025 at 02:00 PM
https://www.instagram.com/p/DF5Q7OCtHMY/?igsh=aGF4ZDl6b3hkbGh4
*Gharama za uendeshaji wa Air Tanzania zafikia 17%, PIC Yapendekeza Serikali Kuharakisha Uhamishaji wa umiliki wa Ndege.*
Gharama za uendeshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) zimetajwa kuongezeka kwa asilimia 17 ndani ya miaka mitatu mfululizo, huku asilimia 95 ya madeni yake yakihusiana na ukodishaji wa ndege kutoka Mfuko wa Fedha za Kigeni (TGFA).
Kufuatia hali hiyo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imependekeza Serikali kuharakisha mchakato wa kuhamisha umiliki wa ndege kutoka kwa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) kwenda ATCL ili kupunguza mzigo wa madeni na kuimarisha utendaji wa shirika hilo.
Akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo bungeni jijini Dodoma leo Februari 10, 2025, Mwenyekiti wa PIC, Augustine Holle, alisema licha ya Serikali kuwekeza katika ununuzi wa ndege 15 kwa fedha taslimu, hali ya kifedha ya ATCL bado inakabiliwa na changamoto.
Kamati imeitaka Serikali kukamilisha haraka uhamishaji wa ndege hizo kwa ATCL ili kuruhusu shirika hilo kupanua huduma zake ndani na nje ya nchi kwa ufanisi zaidi.
.
Chanzo: Mwanachi
#airlines #airtanzania #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv