
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 14, 2025 at 11:37 AM
https://www.instagram.com/p/DGDUFmIN_eS/?igsh=MXZoYXFudDY5ajh5ZA==
*Abiria mjamzito ajifungua ndani ya ndege ya Brussels Airlines muda mfupi baada ya ndege kuanza kupaa.*
Februari 11, 2025 abiria wa ndege ya @flyingbrussels safari namba SN204 kutokea mji wa Dakar kuelekea mji wa Brussels walishuhudia tukio la kipekee baada ya mama mjamzito kujifungua ndani ya ndege hiyo.
Mama huyo, aliyekuwa na ujauzito wa wiki 32, alianza kupata haki ya uchungu wa kujifungua dakika 30 tu baada ya ndege ya Airbus A330 yenye namba ya usajili OO-SFF kupaa. Wahudumu wa ndege walichukua hatua za haraka kwa kumhamishia sehemu ya nyuma ya ndege kwa faragha na kutafuta msaada wa kitabibu.
Miongoni mwa abiria walikuwa katika ndege hiyo alikuwa Lore Nachtergaele, muuguzi mwenye umri wa miaka 22 ambaye amehitimu masomo yake hivi karibuni, pamoja na daktari kijana, ambao walijitokeza kusaidia katika zoezi hilo.
Licha ya rubani kupanga kurudi katika mji wa Dakar, mtoto alizaliwa kabla ya ndege kutua.
Mtoto huyo wa kike, ambaye baadaye aliitwa Fanta, alizaliwa salama bila matatizo yoyote na imeelezwa kuwa mama na mtoto wako waliwasili salama katika mji wa Dakar.
.
##birthonboard #cabincrew #a330 #brusselsairlines #aviationcareer #aviation #aviationlovers #aviatamedia #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania✈