
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 18, 2025 at 02:40 PM
https://www.instagram.com/p/DGN8OZJN4m1/?igsh=cmludXE4azdvZWRt
*Shirika la ndege la Air Tanzania lazindua safari za Dar es salaam- Mtwara,Nauli 199,000*
Shirika la ndege la Air Tanzania leo Februari 18, 2025 limezindua rasmi safari zake katika miji ya Mtwara-Dar es salaam hatua inayotarajiwa kuimarisha uchumi katika mkoa wa Mtwara na mikoa ya Jirani.
Akizungumza katika uzinduzi wa safari hizo,Rubani kiongozi wa Shirika hilo, Captain Arif Jinnah amebainisha kuwa safari hizo zitasaidia kuunganisha wasafiri na mtandao mpana wa Air Tanzania wenye vituo Zaidi ya 25 na miruko Zaidi ya 120 kwa wiki ndani na nje ya nchi.
Gharama za nauli katika safari hiyo zimetajwa kuwa ni kiasi cha shilingi 199,000 huku nauli hizo zikipewa jina la "Samia Fares" (Nauli ya mama)
.
#airlines #airtanzania #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv