Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 22, 2025 at 02:41 PM
https://www.instagram.com/p/DGYPP3kNRQz/?igsh=NHdwNm5hOWR6dmtp *Air Tanzania yarejesha safari za Dar-Iringa baada ya kusitishwa kwa miaka mitano.* Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) limerejesha safari zake za anga kati ya Dar es Salaam na Iringa baada ya kusitisha huduma hiyo kwa takriban miaka mitano tangu Juni 2020. Hatua hii inafuatia kukamilika kwa mradi wa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Iringa, uliogharimu takriban shilingi bilioni 63.742. Ukarabati huo, uliofanywa kwa ushirikiano kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), umekamilika kwa asilimia 95 na kuwezesha kuanza kwa safari hizo mara tatu kwa wiki. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, ameyabainisha hayo katika hafla ya uzinduzi wa safari hizo iliyofanyika leo Februari 22, 2025, mkoani Iringa. Nauli ya safari za Dar es Salaam-Iringa imetajwa kuwa ni shilingi 122,200 kwa safari moja kutoka Dar es Salaam hadi Iringa na shilingi 199,000 safari ya kwenda na kurudi. . #airlines #airtanzania #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania#aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv

Comments