
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 24, 2025 at 05:37 AM
https://www.instagram.com/reel/DGcan4QtCpc/?igsh=bTlqOWI2OXU1OHow
*Tazama Ndege za kivita za Jeshi la Anga la Italia, Eurofighter Typhoon, zikiimarisha ulinzi wa ndege ya American Airlines safari namba AA292 baada ya ndege hiyo kupokea tishio la bomu.*
Ripoti zisizo rasmi zimeeleza kuwa, kuwa bomu lingelipuka ikiwa ndege hiyo ingeshuka chini ya futi 10,000 wakati wa kushuka kuelekea Delhi. Kutokana na tahadhari, wahudumu wa ndege waliamua kugeuza mwelekeo wake walipokuwa wakiruka juu ya Bahari ya Caspian.
Ndege hiyo, aina ya Boeing 787-9 Dreamliner (N480AN), iliyokuwa ikifanya safari kutoka New York kuelekea Delhi, ilikuwa imebeba zaidi ya abiria 280, ililazimika kutua katika Uwanja wa Ndege wa Fiumicino (FCO) huko Roma kwa usalama. Abiria wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo walitolewa salama mara baada ya kutua.
.
#bombthreat #americanairlines #boeing7879 #eurofighertyphoon #airsafety #safety #aircraft #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv