Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 22, 2025 at 03:57 AM
https://www.instagram.com/reel/DJ7LSNsMOdS/?igsh=dGdzeGg3OGYxYWF2 *”Ni Ndege Moja ya Air Tanzania Iliyopo Kwenye Matengenezo Kati ya 16”* Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la @airtanzania_atcl , Mhandisi Peter Ulanga, amesema kuwa kwa sasa ni ndege moja pekee inayofanyiwa matengenezo ya muda mrefu, ambayo yanatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Juni mwaka huu. Mhandisi Peter alieleza hayo katika mahojiano na Shirika la Habari la TBC, ambapo alisema kuwa ndege hiyo imekuwa katika matengenezo kwa kipindi cha miezi sita, huku ndege nyingine 15 zikiendelea kutoa huduma kama kawaida. Ameongeza kuwa matengenezo hayo yanafanyika hapa nchini kwa kushirikiana na wahandisi wa ndani pamoja na msaada wa wahandisi kutoka mashirika mengine pale unapohitajika. Kwa sasa ATCL ina jumla ya ya ndege 16 ambazo ndege hizo ni pamoja na ndege moja aina ya Dash 8-Q300, Dash 8-Q400 tano, Airbus A220-300 nne, Boeing 737 Max 9 mbili, Boeing 787-8 Dreamliner tatu na ndege ya moja ya mizigo aina ya Boeing 767-300F. Video credit: TBC #airline #airtanzania #airtanzania_atcl #aviationcareer #aviationlovers #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Comments