Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 22, 2025 at 08:35 AM
https://www.instagram.com/p/DJ8uejysz9H/?igsh=MTBvbTBiM3pwdW1meQ== *Air Tanzania Yapunguza Ucheleweshaji wa Safari kutoka 80% hadi 10%.* Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Air Tanzania, Mhandisi Peter Ulanga, amesema shirika hilo limepunguza ucheleweshaji wa safari kutoka asilimia 80 hadi asilimia 10. Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la TBC, Mhandisi Ulanga amesema kupunguza ucheleweshaji wa safari ni miongoni mwa vipaumbele alivyoviweka tangu alipoingia katika nafasi ya uongozi, kwa lengo la kurejesha imani kwa abiria. Aidha, amesema kipaumbele kingine ni jitihada za kufufua ndege ambazo zilikuwa katika matengenezo kwa muda mrefu. #flightdelays #airline #airtanzania #airtanzania_atcl #aviationcareer #aviationlovers #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Comments