
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 22, 2025 at 11:26 AM
https://www.instagram.com/p/DJ9D3MhsIiH/?igsh=aDhudnA2eGw3M2Zu
*Kuelekea uzinduzi wa Safari za Arusha–Nairobi, Flightlink yatambuliwa rasmi na na KATA*
Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Kampuni ya ndege ya Flightlink kuzindua rasmi safari kati ya miji ya Arusha-Nairobi,kampuni hiyo imepokea rasmi Cheti na Uanachama kutoka Chama cha Wakala wa Usafiri wa Ndege Kenya (KATA).
Hii ni sehemu ya mafanikio ya kampuni hiyo katika kuhakiki huduma bora na za kuaminika kwa wateja wake.
Kupitia uanachama huu, Flightlink sasa inatambuliwa rasmi kama mshirika wa KATA chama cha kitaaluma kinachowakilisha na kusimamia maslahi ya mawakala wa usafiri nchini Kenya.
Flightlink inatarajia kuzindua safari za anga kati ya mji wa Arusha na Nairobi kuanzia mwezi juni 15,2025 ,Safari ambazo zinalenga kurahisisha usafiri kwa wasafiri wa kibiashara, watalii, na wale wanaosafiri kwa shughuli binafsi.
#airline #flightlink #kata #routeexpansion #aviationlovers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates