Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 2, 2025 at 10:06 AM
https://www.instagram.com/p/DKZPgzoMsxD/?igsh=YTdveW5ndnF5ZnRt *TAA yatangaza kuanza Kwa safari mpya za shirika la ndege la Flightlink.* Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania @tanzaniairports imetangaza kuanza kwa safari mpya za anga za shirika la ndege la @flightlinktz kati ya miji ya Arusha na Nairobi, kuanzia tarehe 15 Juni 2025. Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na TAA, Flightlink itaanzisha safari ya kila siku kutoka Arusha kwenda Nairobi, ikiwa ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za usafiri wa anga katika ukanda wa Kaskazini mwa Tanzania. Katika maandalizi ya safari hizo,TAA ikishirikiana na Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, iko mbioni kukamilisha mfumo wa upokeaji na upangaji wa maafisa wa uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Arusha ili kuhakikisha safari hizo zinafanyika kwa ufanisi. TAA imesisitiza kuwa inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri wa anga kuhakikisha huduma bora kwa abiria na kuwezesha maoni kutoka kwa watumiaji wa viwanja vyake ili kuboresha huduma zaidi. #airlines #flightlink #aviationlovers #aviationcareer #ys #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Comments