
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 14, 2025 at 06:34 AM
https://www.instagram.com/reel/DK3wZNyNkpC/?igsh=eXBma3ExaXYwbDhh
*Jaribio la kwanza la kutua Kwa ndege lafanyika katika kiwanja cha ndege cha kimataifa, Msalato.*
Siku ya Jana Juni 13,2025, ndege aina ya Bombardier Q 400 inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL), imetua kwa mafanikio katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya majaribio ya ufanisi wa kiwanja hicho kipya.
Hili linakuwa ni jaribio la kwanza la kutua kwa ndege ya kibiashara katika kiwanja hicho ambacho kipo katika hatua za mwisho za maandalizi kabla ya kuanza rasmi kwa shughuli za usafiri wa anga.
Kukamilika kwa kiwanja cha Ndege cha Msalato kutaiwezesha Tanzania kuwa na jumla ya viwanja vya ndege 62, ambapo vitatu kati yake vitakuwa ni viwanja vya kimataifa.
#airport #tanzaniaairportsauthority #msalatointernationalairport #mia #atcl #q400 #aviationupdate #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzanianews