Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 17, 2025 at 06:11 PM
https://www.instagram.com/p/DGLvaWRNkaQ/?igsh=cHd4YW5xYWNhYTcx *TCAA yasisitiza udhibiti wa matumizi ya "drones" kwa usalama wa anga Tanzania.* Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetoa onyo kali kwa watumiaji wa ndege zisizo na rubani (drones), ikisisitiza kuwa matumizi yasiyo na vibali yanaweza kuhatarisha usalama wa anga. Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw.Salim Msangi, amebainisha kuwa kumekuwepo na ongezeko la matumizi holela ya drones,kwa watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, hali inayokiuka sheria na kutishia usalama kwa safari za anga. Bwana Msangi amezungumza hayo,leo Februari 17, 2025, katika hafla ya kukabidhi misaada kwa wafungwa wa Gereza Kuu la Karanga, Moshi na kuongeza kuwa sheria inawataka watumiaji wa drones kupata vibali maalum kabla ya kuzitumia. Ameeleza kuwa drones zinapaswa kusajiliwa kama ilivyo kwa ndege nyingine, na matumizi yake lazima yaidhinishwe na mamlaka husika. Msangi amesisitiza kuwa maeneo nyeti kama magereza na taasisi za kijeshi ni marufuku kurusha ndege za drones, na yeyote atakayekiuka sheria atachukuliwa hatua kali, ikiwemo kushtakiwa. Pia, ameonya kuwa matumizi yasiyodhibitiwa yanaweza kusababisha ajali za anga, akitoa tahadhari dhidi ya uwezekano wa drones kugongana na ndege kubwa zinazobeba abiria. . #airlines #tcaa #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania#aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv

Comments