
Aviation Tanzania 🇹🇿
February 12, 2025 at 08:52 AM
https://www.instagram.com/p/DF924x6tO1a/?igsh=MXRkNm5xZHVqYzEzaQ==
*Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania wajifunza kuhusu ndege za kijeshi za MV-22 Osprey.*
Wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania wamepata fursa ya kutembelea ndege za kijeshi za Marekani aina ya MV-22 Osprey, na kupokea maelezo ya kina kutoka kwa marubani wa jeshi la Marekani kuhusu uwezo na muundo wa ndege hizo za kipekee.
Ndege hizo hutumika kwa mazoezi ya kijeshi yajulikanayo kama Justified Accord 2025,mazoezi yanayohusisha vikosi vya jeshi la nchi kavu kutoka Tanzania na Marekani kwa mafunzo ya pamoja ya Operesheni za Usaidizi wa Amani.
Ushirikiano huu wa kijeshi unalenga kuimarisha usalama wa kikanda na kuendeleza mahusiano kati ya Tanzania na Marekani katika sekta ya ulinzi na usalama.
.
@usembassytz
#usembassy #mv22osprey #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv