Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 23, 2025 at 07:58 AM
https://www.instagram.com/reel/DJ_P3Qas5B2/?igsh=ZDNzY2o3cnBqb3Z4 *Air Tanzania yajipanga kuanza safari za ndani na nje ya nchi Katika maeneo haya.* Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la @airtanzania_atcl , Mhandisi Peter Ulanga, ametaja maeneo kadhaa ndani na nje ya nchi yanayohitaji kwa kiwango kikubwa huduma ya usafiri wa anga, akieleza kuwa tayari imeanza kuweka mipango kwa ajili ya kufanikisha huduma hizo. Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la TBC, Mhandisi Ulanga alisema kuwa ndani ya nchi, maeneo ya Musoma, Shinyanga na hasa Bukoba yanaonesha uhitaji mkubwa wa huduma za ndege na kubainisha kuwa Bukoba ndiyo eneo lenye mahitaji ya juu zaidi, huku serikali ikiwa tayari imewekeza katika ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika maeneo hayo. Kwa upande wa safari za kimataifa, Mhandisi Ulanga alieleza kuwa taifa jirani la Msumbiji limeomba Air Tanzania kuanzisha safari zake kuelekea miji ya Maputo, Beira, Nampula na Pemba. Aidha, shirika hilo pia linaangazia uwezekano wa kuanzisha safari kuelekea visiwa vya Mayotte na Shelisheli, maeneo maarufu kwa vivutio vya utalii na biashara. Katika mipango yake ya ndani zaidi, Air Tanzania inatarajia kufungua safari za moja kwa moja kuelekea visiwa vya Pemba, Mafia na hifadhi ya Serengeti, hasa wakati wa msimu wa utalii, hatua ambayo inalenga kuimarisha utalii wa ndani na kuongeza mapato kwa taifa. Hadi sasa, Shirika la Ndege la ATCL linahudumia maeneo 14 ndani ya nchi. Katika bara la Afrika, linatoa huduma katika vituo 10, na nje ya Afrika linafika katika vituo vitatu. #routeexpansion #airline #airtanzania #airtanzania_atcl #aviationcareer #aviationlovers #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Comments