YESU NI JIBU WhatsApp Channel

YESU NI JIBU

121 subscribers

About YESU NI JIBU

Chanell hili ni maalumu kwa ajili ya kutuweka pamoja chini ya Yesu Kristo kupitia roho mtakatifu, Kufunua mapenzi ya Mungu kwetu, Mafundisho ya Imani, wokovu, Ukombozi na Maombi. 🌑mambo ya Misingi katika group hili. 👉Maombi na Maombezi 👉Neno 👉Mafunuo 👉Injili, mahubiri na Mafundisho. 👉Maswali na majibu ISAYA 65:24--Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia. 1 Peter 5:7--huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

Similar Channels

Swipe to see more

Posts

YESU NI JIBU
YESU NI JIBU
2/20/2025, 4:53:57 AM

Mungu anakuona, Mungu anakusikia, Mungu Yuko tayari kutenda jema SIKU ya leo, Mtukuze kwa aliyowahi kufanya juu yako. *Zaburi 150:6* ---Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA. Haleluya. #YesuNiJibu #WokovuNiSasa

Image
YESU NI JIBU
YESU NI JIBU
2/19/2025, 6:26:45 AM

Mungu anayajua unayoyapitia, Omba kushinda mitihani hiyo naye atakutukuza hakika, wewe ni Mshindi *Ayubu 23:10--* Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. #YesuNiJibu #WokovuNiSasa

🙏 1
Image
YESU NI JIBU
YESU NI JIBU
2/23/2025, 6:51:30 AM

Ifanye JPILI yako kuwa takatifu, Mkumbuke Muumba wako Kwa matendo makuu anayekutedea, Mshangilie moyoni mwako. *Kutoka 20:8--* Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. #YesuNiJibu #WokovuNiSasa

Image
YESU NI JIBU
YESU NI JIBU
2/21/2025, 3:48:42 AM

Siku ya leo BWANA atakuangazia nuru za uso wako, atakulipa fadhili, atawapiga Adui zako na kukupa Amani, hakika atatembea nawe. Amini Amini Bwana atafanya haya kwa ajili yako, Kilio chako kimesikika. *Kutoka 33:14* --Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. #YesuNiJibu #WokovuNiSasa

❤️ 1
Image
YESU NI JIBU
YESU NI JIBU
2/17/2025, 4:36:44 AM

Wiki yako ikawe ya Baraka na mafanikio, BWANA akawe msaada wako kwa kila uliwazalo na kufanya. *Zaburi 121:2--* Msaada wangu u katika BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi. #YesuNiJibu

🙏 1
Image
YESU NI JIBU
YESU NI JIBU
2/22/2025, 2:58:30 AM

Kitu chochote unachokipitia, kisicho ondoa roho yako jua kina kuimalisha. Kuwa na furaha tupu na kumshukuru Mungu kwa unayoyapitia, hakika utaona wema wa BWANA. *Yakobo 1:2--* Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; #YesuNiJibu #WokovuNiSasa

🙏 1
Image
YESU NI JIBU
YESU NI JIBU
2/25/2025, 5:46:00 AM

Wema ni akiba mbele za Mungu, tendea watu mema SIKU zote. BWANA uwapa upedeleo (Neema) watendao mema, wabeba mzigo ya Wengine. *Mithali 12:2--Mtu* mwema atapata upendeleo kwa BWANA; Bali mtu wa hila atahukumiwa naye. #YesuNiJibu #WokovuNiSasa

🙏 1
Image
YESU NI JIBU
YESU NI JIBU
2/24/2025, 3:18:07 AM

Mungu wetu si kipofu asione unayoyapitia, si kiziwi asisikie haja za moyo yako. Mungu anajali sana juu yako, omba pasipo kukata maa atatenda kwa majira yake. *Yeremia 29:12--* Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.

🙏 1
Image
YESU NI JIBU
YESU NI JIBU
2/18/2025, 4:43:36 AM

Je unajua kuwa Mungu ni BWANA wako!? Mtii na kumtumikia naye atakuokoa katika tabu zako na kukuinua juu zaidi. *Isaya 43:11* --Mimi, naam, mimi, ni BWANA, zaidi yangu mimi hapana mwokozi. #YesuNiJibu #WokovuNiSasa

Image
YESU NI JIBU
YESU NI JIBU
2/16/2025, 7:21:19 AM

*Unataka Yesu leo akutendee Nini??* Omba lolote naye atafanye, omba kwa imani *Yohana 3:36--* Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia. #YesuNiJibu

🙏 1
Image
Link copied to clipboard!